Kufikia sasa watu 24 wamefariki kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi nchini Kenya
Tume ya kitaifa ya kutetea haki za kibinadamu, KNCHR inasema kufikia sasa watu 24 wamefariki kutokana na vurugu za baada ya uchaguzi nchini Kenya. Naibu Mwenyekiti George Morara anasema tume hiyo ina waangalizi 264 ambao wamekuwa wanafuatilia matukio ya baada ya uchaguzi katika kaunti 37 na wao ndio wamekuwa wakiwapa takwimu hizo .