Filamu ya Kitanzania yapaa anga za kimataifa
Sekta ya filamu imeendelea kukua kila kukicha nchini Tanzania,ambapo sasa filamu zinazotengenezwa nchini humo zinavuka anga ya kimataifa na kuonyeshwa sehemu nyingine duniani.
T Junction ni miongoni mwazo, na licha ya kwamba imeigizwa na vijana chipukizi lakini maudhui yake yameweza kugusa wengi.