Kwa Picha: Foleni, mitindo na bashasha Uchaguzi Mkuu Kenya 2017

Wapiga kura nchini Kenya walishiriki uchaguzi mkuu Jumanne, baadhi wakifika mapema sana kabla ya vituo kufunguliwa. Kuna wale waliofika kwa mitindo ya aina yake na wengine wakatumia mkusanyiko wa watu kama fursa ya kibiashara.

Nairobi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu walianza kupanga foleni nje ya vituo mapema
Uwanja wa Mbuzi
Maelezo ya picha, Hivi ndivyo hali ilivyokuwa katika kituo cha kupigia kura cha Uwanja wa Mbuzi katika uwanja wa michezo wa Mombasa.
Raul
Maelezo ya picha, Wakati watu wakiwa kwenye foleni wakisubiri kupiga kura jijini Nairobi, Kenya kibaridi kikali kimetoa fursa ya kibiashara kwa mchuuza kahawa huyu kwa jina Raul.
Zuia Noma
Maelezo ya picha, mwanamume huyu amekuwa akiwahimiza kudumisha amani wakati wa uchaguzi wenyewe na baadaye. Mwandishi wetu Abdinoor Aden alikutana naye karibu na kituo cha Olympic mtaa wa Kibera, Nairobi.
Rais Kenyatta
Maelezo ya picha, Rais Kenyatta alipiga kura yake kituo cha Mutomo eneo lake la nyumbani la Gatundu, kaskazini mwa Nairobi.
Kenyatta
Maelezo ya picha, Baada ya kupiga kura yake, alisema kwamba yuko tayari kukubali matokeo ya uchaguzi huo.
Raila Odinga

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mgombea wa upinzani Raila Odinga alipiga kura yake katika mtaa wa Kibra, Nairobi ambapo alisemasema kuwa anahofia huenda kukatokea wizi wa kura
Raila Odinga
Maelezo ya picha, Wanahabari na kamera zao walikuwa wamemzunguka akipiga kura
Kibra, Nairobi
Maelezo ya picha, Nje wakazi walijaribu kutumia kila njia kumuona akipiga kura...
Kibra, Nairobi
Maelezo ya picha, ...wengine nao wakajaribu kujiwekea kumbukumbu kupitia simu zao za rununu.
Naibu Rais William Ruto akipiga kura katika kituo cha Kosachei, katika kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya
Maelezo ya picha, Naibu Rais William Ruto alipiga kura katika kituo cha Kosachei, katika kaunti ya Uasin Gishu magharibi mwa Kenya.
Ruto
Maelezo ya picha, Bw Ruto alitembea kutoka nyumbani kwake hadi kituo cha kupigia kura. Njiani, alimpata mzee huyu akipumzika na akachukua muda kumjulia hali.
Kusaidiwa
Maelezo ya picha, Wapiga kura wasioweza kusoma na kuandika, walisaidia kufanya uamuzi, kama ilivyokuwa kwa bibi huyu kituo cha Kosachei.
Vidole Kibera
Maelezo ya picha, Baada ya kupiga kura, mpiga kura alikuwa akipakwa wino usiofutika kwa urahisi kwenye kidole kuzuia watu kurejea mara ya pili.
Eldoret
Maelezo ya picha, Serikali ilikuwa imetangaza leo kuwa sikukuu kuwapa wananchi fursa ya kupiga kura na katika miji mingi maduka na afisi nyingi zilifungwa. Hata hivyo, baadaye mchana baadhi ya wafanyabiashara walifungua biashara zao, mfano mwanamke huyu mjini Eldoret.
Ahmed Noor Mohammed
Maelezo ya picha, Baadhi ya waliotaka kupiga kura hawakubahatika, mfano huyu Ahmed Noor Mohammed mtaa wa Eastleigh ambaye jina lake halikupatikana katika sajili kituo alichofika kutaka kupiga kura.
Kerry
Maelezo ya picha, Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ni miongoni mwa waangalizi wanaofuatilia uchaguzi mkuu Kenya. Hapa, alikuwa katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya Moi Avenue, Nairobi
Makonde
Maelezo ya picha, Watu wa jamii ya Wamakonde walikuwa wanapiga kura kwa mara yao ya kwanza kabisa, baada ya kutambuliwa kama Wakenya miezi michache iliyopita. Doto Nguli, 28, alikuwa miongoni mwa watu wa jamii hiyo waliopiga kura kituo cha Wabungo katika kaunti ya Kwale, pwani ya Kenya.
Kibera
Maelezo ya picha, Mwanamume huyu mtaa wa Kibera hakuficha siri yake kuhusu nani anamuunga mkono kinyang'anyiro cha urais...
Uzalengo
Maelezo ya picha, Watatu hawa nao wakafika Gatundu wakiwa wamevalia mavazi yenye rangi za bendera ya Kenya, labda kuonesha uzalendo.