Picha: Waislamu walivyosherehekea Eid ul-Fitr duniani

Waislamu pande zote za dunia washerehekea siku kuu ya Eid kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan

Hapa ni katika kijiji cha Dalgamon nchini Misri, kilomita 120 kaskazini mwa Cairo wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid tarehe 25 Juni.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Maadhimisho ya siku kuu ya Eid yalianza Jumapili Misri na mataifa mengine ya Kiarabu, baada ya mwezi kuonekana rasmi. Hapa ni katika kijiji cha Dalgamon nchini Misri, kilomita 120 kaskazini mwa mji wa Cairo.
Msichana huyu ni miongoni mwa raia wengi wa mji wa Mosul Iraq wanaosherehekea siku kuu ya Eid bila udhibiti wa kundi la Islamic state.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Msichana huyu alijipamba vilivyo wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid katika mji wa Mosul. Ni miongoni mwa raia wa Mosul wanaosherehekea siku kuu Eid bila udhibiti wa kundi la Islamic state nchini Iraq baada ya miaka mingi.
Waumini wa kiislamu waondoka msikiti wa Blue Mosque baada ya maombi ya Eid al-Fitr mjini Istanbul tarehe 25 Juni

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waumini hawa waliadhimisha siku kuu ya Eid katika msikiti maarufu wa Blue Mosque mjini Istanbul, Uturuki.
Rais wa Syria Bashar al-Assad (wa pili kutoka kushoto) ahudhuria ibada ya maombi mjini Hama tarehe 25 Juni.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais wa Syria Bashar al-Assad (wa pili kutoka kushoto), ambaye anaendelea kushikilia maamlaka baada ya miaka sita ya mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe, ashiriki maombi ya kuadhimisha siku kuu ya Eid katika mji wa Hama
Waislamu nchini Palestina wahudhuria ibada ya maombi, tarehe 25 Juni, katika uwanja mjini Gaza.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Akina mama na wasichana wa Kiislamu katika ibada ya Eid, Gaza, Palestina. Misri ilianza kupeleka mafuta ya kuendesha kituo cha kuzalisha umeme mjini Gaza wiki hii na kutatua mzozo wa malipo uliotishia kusambaratisha sherehe za Eid.
Waumini wa dini ya Kiislamu waomba kwenye barabara ya Moscow tarehe 25 Juni.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waislamu mjini Moscow Russia walishiriki maombi barabarani karibu na msikiti mkuu. Moscow haina maeneo ya kutosha ya ibada kwa Waislamu, ambao asilimia kubwa ni wahamiaji kutoka katikati mwa Asia.
Waumini wa kiislamu kutoka jamii ya Southwark's wapigwa picha wakiadhimisha siku kuu ya Eid katika bustani ya Dulwich, London tarehe 25 Juni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waislamu hawa mjini London waliadhimisha siku kuu ya Eid katika bustani ya Dulwich.
Waislamu wa Misri waachilia puto hewani baada ya maombi mjini Cairo

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waislamu wa Misri waachilia puto hewani baada ya maombi mjini Cairo
Wanawake wakumbatiana wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid katika uwanja wa mji wa Anaheim, California

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Nchini Marekani, Waislamu walikongamana katika uga wa Anaheim, California.
Wanawake wa Kiislamu waondoka msikiti wa mji wa Marawi Ufilipino baada ya kuadhimisha siku kuu ya Eid al-Fitr tarehe 25 Juni

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Ufilipino wametangaza kusitisha mapigano kwa muda dhidi ya magaidi wa Islamic State katika mji wa kiislamu wa Marawi.
Dhifa ya kufuturu Mexico City

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Waumini wa Kiislamu wapanga foleni ili kupata futari Mexico City.
Msichana aonyesha mapambo ya hena wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid Karachi, Pakistan.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Msichana aonyesha mapambo ya hena wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya Eid Karachi, Pakistan.