Kwa Picha: Meli ya kivita ya Marekani USS Fitzgerald ilivyoharibiwa

Picha za uharibifu uliotokea baada ya meli ya kivita ya Marekani USS Fitzgerald kugongana na meli ya mizigo

USS Fitzgerald Juni 17, 2017

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Manowari ya USS Fitzgerald iligongana na meli ya kubeba mizigo mwendo wa saa nane unusu usiku wa manane saa za Japan Jumamosi.
USS Fitzgerald

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Ajali hiyo ilisababisha maji kufurika katika meli hiyo ya Marekani. Wanabaharia saba walitoweka.
USS Fitzgerald Juni 17, 2017.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Meli hiyo, ikiwa imeharibiwa, ilirejea pole pole ikisaidiwa na boti kadha hadi katika kambi ya majeshi ya Marekani Yokosuka
USS Fitzgerald,

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Haijabainika ilitokea vipi meli hiyo ya kivita, ambayo ni moja ya meli zenye mitambo ya kisasa zaidi duniani, ikagongana na meli hiyo ya mizigo.
USS Fitzgerald

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Watu watatu, akiwemo kamanda mkuu wa meli hiyo, walilazwa hospitalini.
USS Fitzgerald

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Ajali hiyo ilitokea eneo lenye maji matulivu, na hali ya anga ilikuwa nzuri.
ACX Crystal

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Meli ya mizigo iliyogongana na meli hiyo ya Marekani, ACX Crystal ambayo imesajiliwa Ufilipino, haikuharibiwa sana
USS Fitzgerald

Chanzo cha picha, Kyodo via Reuters

Maelezo ya picha, ACX Crystal iliendelea na safari yake hadi Tokyo
Meli hiyo ya Ufilipino ilikuwa na uzani karibu mara tatu ukilinganisha na meli hiyo ya Marekani.
Maelezo ya picha, Meli hiyo ya Ufilipino ilikuwa na uzani karibu mara tatu ukilinganisha na meli hiyo ya Marekani.
Ramani ya safari ya meli hiyo ya Ufilipino na eneo ambalo meli hizo mbili ziligongana.
Maelezo ya picha, Ramani ya safari ya meli hiyo ya Ufilipino na eneo ambalo meli hizo mbili ziligongana.