Picha: Kituo cha Nairobi cha reli ya kisasa SGR

Treni inayotumia reli ya kisasa iliyozinduliwa Kenya na rais Uhuru Kenyatta ambayo imepewa jina la Madaraka Express Kenyatta imeanza safari nchini humo.

Reli ya kisasa ya SGR nchini Kenya iliyozinduliwa ilikuwa ni matokeo ya maafikiano kati ya Serikali ya Kenya na China ambapo China ilifadhili asilimia 80 na Kenya ikafadhili asilimia 20 iliyobaki.
Maelezo ya picha, Reli ya kisasa ya SGR nchini Kenya iliyozinduliwa ilikuwa ni matokeo ya maafikiano kati ya Serikali ya Kenya na China ambapo China ilifadhili asilimia 80 na Kenya ikafadhili asilimia 20 iliyobaki.
Kenya ilijiunga na nchi nyingine 67 katika mradi wa miundombinu ya gharama ya shilingi trilioni 15 inayofadhiliwa na Uchina. Kila nchi itajitetea kivyake kupata fedha za kugharamia miundombinu hiyo kutoka kwa mpango huu.
Maelezo ya picha, Kenya ilijiunga na nchi nyingine 67 katika mpango mkubwa wa miradi ya miundombinu ya gharama ya shilingi trilioni 15 inayofadhiliwa na Uchina. Kila nchi itajitetea kivyake kupata fedha za kugharamia miundombinu hiyo kutoka kwa mpango huu.
Kenya ilifaulu kupata mkopo huo ambao nchi hiyo imepewa kipindi cha miaka 10 kabla ya kuanza kulipa, baada ya reli hiyo kuanza kupata mapato. Halafu baadaye malipo yake yatafanywa kwa kati ya miaka 30-40.
Maelezo ya picha, Kenya ilifaulu kupata mkopo huo ambao nchi hiyo imepewa kipindi cha miaka 10 kabla ya kuanza kulipa, baada ya reli hiyo kuanza kupata mapato. Halafu baadaye malipo yake yatafanywa kwa kati ya miaka 30-40.
Treni hiyo ya kisasa inauwezo wa kuenda mwendo wa kilomita 120 kwa kila saa huku barabara ya reli kutoka Mombasa kuelekea Nairobi ikiwa na urefu wa kilomita 472
Maelezo ya picha, Treni hiyo ya kisasa inauwezo wa kuenda mwendo wa kilomita 120 kwa kila saa huku barabara ya reli kutoka Mombasa kuelekea Nairobi ikiwa na urefu wa kilomita 472
Hii ni awamu ya kwanza kukamilika na inaunganisha Mombasa na Nairobi, mradi ambao uliwagharimu Wakenya dola bilioni 3.2.
Maelezo ya picha, Hii ni awamu ya kwanza kukamilika na inaunganisha Mombasa na Nairobi, mradi ambao uliwagharimu Wakenya dola bilioni 3.2.
Awamu ya pili 2(a) itaunganisha Nairobi na Naivasha na itagharimu dola bilioni 1.5.
Maelezo ya picha, Awamu ya pili 2(a) itaunganisha Nairobi na Naivasha na itagharimu dola bilioni 1.5.
Awamu ya mwisho 2(b) itakayounganisha Naivasha – Kisumu – Malaba ikigharimu dola 3.5 bilioni.
Maelezo ya picha, Awamu ya mwisho 2(b) itakayounganisha Naivasha – Kisumu – Malaba ikigharimu dola 3.5 bilioni.
Kwa sasa China inatekeleza majukumu yote ya reli hiyo. Hata hivyo kuna vijana Wakenya wanaopewa mafunzo katika taaluma tofauti nchini China. Kenya inatarajiwa kuchukua usukani baada ya miaka mitano.
Maelezo ya picha, Kwa sasa China inatekeleza majukumu yote ya reli hiyo. Hata hivyo kuna vijana Wakenya wanaopewa mafunzo katika taaluma tofauti nchini China. Kenya inatarajiwa kuchukua usukani baada ya miaka mitano.
Mmoja wa nahodha wanawake walioendesha gari moshi lililombemba rais Uhuru Kenyatta kutoka Mombasa hadi Nairobi wakati wa uzinduzi.
Maelezo ya picha, Mmoja wa wahudumu wanawake waliokuwa wanahudumia wateja kwenye gari moshi lililombemba rais Uhuru Kenyatta kutoka Mombasa hadi Nairobi wakati wa uzinduzi.
mtumishi msichana wa treni akiwaashiria abiria mahala pa kuabiria.
Maelezo ya picha, Mhudumu wa treni akiwaashiria abiria mahala pa kupanda treni.
Mahala pa kungojea gari la moshi katika kituo cha Nairobi. Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 700 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.
Maelezo ya picha, Mahala pa kungojea gari moshi katika kituo cha Nairobi. Nauli ya watu watakaokalia viti vya kawaida ni shilingi 700 huku wale watakaosafiri kwa kutumia business class wakilipa shilingi 3,000.
Njia inayoelekeza mahala pa kuabiria gari la moshi katika kituo cha Nairobi.
Maelezo ya picha, Njia inayoelekea mahala pa kuabiria gari la moshi katika kituo cha Nairobi.
Winchi ya kubeba mizigo na kuweka katika magari ya moshi ya kubeba mizigo ambayo itabeba kasha la fiti 20 kwa shilingi 50,000 kutoka Mombasa hadi Nairobi.
Maelezo ya picha, Winchi ya kuinua mizigo na kuweka katika magari ya moshi ya kubeba mizigo ambayo yatabeba makasha ya futi 20 kwa shilingi 50,000 kutoka Mombasa hadi Nairobi. Picha zote Peter Njoroge, BBC
Ulinzi umepewa kipao mbele katika vituo vya gari moshi Nairobi na Mombasa.
Maelezo ya picha, Ulinzi umepewa kipao mbele katika vituo vya gari moshi Nairobi na Mombasa.
Wakenya walimiminika katika kituo cha gari la moshi la Nairobi kujionea treni ya kisasa ya SGR iliyozinduliwa
Maelezo ya picha, Wakenya walimiminika katika kituo cha gari la moshi la Nairobi kujionea treni ya kisasa ya SGR iliyozinduliwa