Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria

Maelezo ya sauti, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda katika shinikizo la kuchukuliwa hatua za kisheria

Nchini Tanzania , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameingia katika shinikizo la kutakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria baada ya tuhuma kwamba alivamia ofisi za kituo cha televisheni na radio cha Clouds huku akiwa na askari waliobeba silaha.

Tukio hili ni muendelezo wa shutuma za kugushi vyeti ambazo zimekuwa zikimuandama bwana Makonda kwa wiki kadhaa sasa. Mwandishi wetu Esther Namuhisa anasimulia zaidi kutoka Dar es Salaam