Kwa Picha :Tazama mabondia wa Tanzania walivyorambishwa sakafu na Wakenya

Mashindano ya ndondi katika madaraja tofauti kanda ya Afrika chini ya chama cha ndondi cha Africa Boxing.

Ignas hakuweza kuendelea na pigana na alisalimu amri raundi ya tano
Maelezo ya picha, Ignas hakuweza kuendelea na pigana na alisalimu amri raundi ya tano
Bondia kutoka nchini Tanzania Salehe Mkalekwa (Welterweight), akiwa anashangaa ni nini kilichotendeka baada ya kulambishwa sakafu na Mkenya Rayton Okwiri .
Maelezo ya picha, Bondia kutoka nchini Tanzania Salehe Mkalekwa (Welterweight), akiwa anashangaa ni nini kilichotendeka baada ya kulambishwa sakafu na Mkenya Rayton Okwiri .
Mkenya Rayton Okwiri alinyakuwa ukanda wa Africa kitengo cha Welterweight alipomwangusha Mtazania Salehe Mkalekwa katika raundi ya tatu .
Maelezo ya picha, Mkenya Rayton Okwiri alinyakuwa ukanda wa Africa kitengo cha Welterweight alipomwangusha Mtazania Salehe Mkalekwa katika raundi ya tatu .
Salehe Mkalekwa akiwa amelala chini baada ya ngumi nzito kutoka kwa Okwiri.
Maelezo ya picha, Salehe Mkalekwa akiwa amelala chini baada ya ngumi nzito kutoka kwa Okwiri.
Mkalekwa akisaidiwa na refa kuamka.
Maelezo ya picha, Mkalekwa akisaidiwa na refa kuamka.
Mkenya Nick ‘Kanyankole” Otieno akimenyana na Mtazania Haji Juma katika shindano la Super Flyweight, Nick aliibuka mshindi na kunyakuwa ukanda uliokuwa wazi.
Maelezo ya picha, Mkenya Nick ‘Kanyankole” Otieno akimenyana na Mtazania Haji Juma katika shindano la Super Flyweight, Nick aliibuka mshindi na kunyakuwa ukanda uliokuwa wazi.
Mtanzania Haji Juma , akiwashikuru mashabiki waliojazana ukumbi wa Glown Plaza.
Maelezo ya picha, Mtanzania Haji Juma , akiwashukuru mashabiki waliojazana ukumbi wa Glown Plaza.
Nick ‘Kanyankole” Otieno akiwa na ukanda aliyoshinda .
Maelezo ya picha, Nick ‘Kanyankole” Otieno akiwa na ukanda aliyoshinda .
Mkenya Gabriel Otieno(Kulia) na Mtazania Fadhili Majiha wakipewa mawaidha kabla ya pigano lao la ukanda wa Africa kitengo cha Bantamweight.
Maelezo ya picha, Mkenya Gabriel Otieno(Kulia) na Mtazania Fadhili Majiha wakipewa mawaidha kabla ya pigano lao la ukanda wa Africa kitengo cha Bantamweight.
Gabriel Otieno hakuwa na lake mbele ya Fadhili Majiha aliye mponda kisawasawa na kushinda.
Maelezo ya picha, Gabriel Otieno hakuwa na lake mbele ya Fadhili Majiha aliye mponda kisawasawa na kushinda.
Fadhili alionyesha mchezo wa hali ya juu na kufungua jeraha katika paja la uso la Otieno aliyevuja damu kwa wingi.
Maelezo ya picha, Fadhili alionyesha mchezo wa hali ya juu na kufungua jeraha katika paja la uso la Otieno aliyevuja damu kwa wingi.
Gabriel Otieno akiwaza ni mbinu gani atatumia dhidi ya Fadhili.
Maelezo ya picha, Gabriel Otieno akiwaza ni mbinu gani atatumia dhidi ya Fadhili.
Ingawa Otieno alijitahidi, Fadhili alikuwa mwepesi kwa kila njia.
Maelezo ya picha, Ingawa Otieno alijitahidi, Fadhili alikuwa mwepesi kwa kila njia.
Fadhili Majima akimtandika Gabriel Otieni makonde mazito
Maelezo ya picha, Fadhili Majima akimtandika Gabriel Otieni makonde mazito
Fadhili Majiha ni bondia aliye na uzoefu kwenye ulingo wa ndondi, akiwa ameshiriki kwenye mechi kadha za kulipwa ikiwemo nchini Ufilipino
Maelezo ya picha, Fadhili Majiha ni bondia aliye na uzoefu kwenye ulingo wa ndondi, akiwa ameshiriki kwenye mechi kadha za kulipwa ikiwemo nchini Ufilipino
Fadhili Majiha akiwa na ukanda aliyoshinda .
Maelezo ya picha, Fadhili Majiha akiwa na ukanda aliyoshinda .
Mkenya Dennis ‘Bilabong’ Okoth akimenyana na Mtazania Shadrack Ignas kitengo cha super lightweight.
Maelezo ya picha, Mkenya Dennis ‘Bilabong’ Okoth akimenyana na Mtazania Shadrack Ignas kitengo cha super lightweight.
Shadrack Ignas akilalama kwa refa Mohammed Abdalla Kent kuhusu jeraha kichwani mwa Okoth
Maelezo ya picha, Shadrack Ignas akilalama kwa refa Mohammed Abdalla Kent kuhusu jeraha kichwani mwa Okoth