Wasanii, polisi mbaroni kwa tuhuma za mihadarati Tanzania

Maelezo ya sauti, Wasanii, polisi mbaroni kwa tuhuma za mihadarati Tanzania

Polisi nchini Tanzania inawashikilia watu zaidi ya 10 wakiwemo wasanii maarufu na polisi waliotajwa hapo jana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.

Miongoni mwa watu hao wanaohojiwa yupo msaanii maarufu na miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu, aliyeitikia wito wa polisi pamoja wasanii wenzake kufika kwa mahojiano.

Hapo jana mkuu wa Mkoa huo wa Dar es Salaam nchini humo, Paul Makonda aliwataja watu kadhaa kuhusika na biashara hiyo na kuwataka leo waripoti katika kituo cha polisi.

Kutoka jijini Dar es Salaam Lizzy Masinga na maelezo zaidi.