Umaarufu wa jina Obama magharibi mwa Kenya
Magharibi mwa Kenya, jamii nyingi huwapa majina watoto wao kutoka kwa jamaa wao walioaga dunia, msimu au kwa upande mwingine kutokana na matukio au majina ya watu maarufu.
Katika jamii ya Waluo jina la Rais Barack Obama, ambaye umaarufu wake ulizuka miaka 10 iliyopita alipogombea na kushinda Useneta nchini Marekani na kisha kutambuliwa kuwa ni mwenye asili wa eneo hilo, ndilo lililokuwa maarufu zaidi mwongo uliopita katika jamii hiyo.
Mwandishi wa BBC Muliro Telewa, aliyetembelea eneo hilo na kutuandalia ripoti ifuatayo.