Obama atokwa na machozi akimshukuru Michelle
Rais wa Marekani Barack Obama alitokwa na machozi akimshukuru mkewe Michelle kwa mchango aliotekeleza kabla na wakati wa kipindi chake kama rais.
Aidha, amewashukuru mabinti zake Malia na Sasha kwenye hotuba yake ya mwisho kama rais wa Marekani mjini Chicago.