Kwa Picha: Harusi 'ghali zaidi' India

Mojawapo ya harusi ghali zaidi duniani imefanyika nchini India, na kugharimu jumla ya upee bilioni 5 ($74m; £59m).

Harusi ya kifahari

Chanzo cha picha, Janardhana Reddy Family

Maelezo ya picha, Harusi ya kifahari imefanyika jimbo la Karnataka, kusini mwa India na iligharimu karibu rupee bilioni 5 ($74m; £59m).
Picha za harusi ya Reddy

Chanzo cha picha, Kashif Masood

Maelezo ya picha, Harusi hiyo ya mfanyibiashara na mtoto wa mwanasiasa wa India G Janardhana Reddy's, Brahmani, imepokelewa kwa ghadhabu na mamilioni ya raia wa India ambao kwa sasa wanakumbana na matatizo ya kifedha.
Bibi Harusi

Chanzo cha picha, Familia ya Janardhana Reddy

Maelezo ya picha, Biarusi alikuwa amevalia sari iliyogharimu rupee milioni 170 ($2.5m; £2m) na akavalia mikufu iliyogharimu rupee milioni 900$13m; £10m), ripoti zimesema
Bwanaharusi

Chanzo cha picha, Familia ya Janardhana Reddy

Maelezo ya picha, Bwana harusi, Rajeev Reddy, 23, anayemiliki biashara ya familia yake kutoka mji wa Hyderabad.
wachezaji wa ngoma ya Samba at the Reddy wedding

Chanzo cha picha, Kashif Masood

Maelezo ya picha, Wachezaji wa ngoma ya Kibrazil ya Samba ni miongoni mwa waliowatumbuiza wageni kwenye harusi hiyo .
Baba, ya bwana harusi na bibi harusi

Chanzo cha picha, Kashif Masood

Maelezo ya picha, Watu wengine kwenye mitandao ya kijamii wamesema si vyema kuishtumu harusi hiyo. Bw Reddy amenukuliwa akisema alifanya malipo ya harusi miezi sita kabla harusi yenyewe - kabla serikali kuzifutilia mbali noti za zamani kama njia ya kukabiliana na ulaji wa rushwa - na aliweka mali yake rehani kwa ajili ya harusi.
Bwanaharusi na Bibi harusi

Chanzo cha picha, Kashif Masood

Maelezo ya picha, Nyota wa Bollyhood waliowatumbuiza wageni kwenye harusi hiyo. Wakosoaji wamesema harusi hiyo ya kifahari ni 'kuonyesha utajiri'.
Sehemu ya hekalu

Chanzo cha picha, Kashif Masood

Maelezo ya picha, Maandalizi katika hekalu la Pangalore yalichukua miezi miwili kukamilika. Maandalizi yalifanyika na walitengeneza madhabahu mfano wa yaliyotumiwa na Wahindi wa kale kwa ajili ya harusi hiyo
Bw Reddy (lkushoto) na mwanawe wa kike na jamaa zake.

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Zaidi ya wageni 50,000 walihudhuria harusi hiyo. Ripoti zimesema teksi 2,000 ziliwabeba wageni na ndege aina ya helikopta 15 ziliwaleta wageni maalum waalikwa.