Mtalii Mmarekani aliyegeuka na kuwa mwenyeji Lamu, Kenya
Mji wa Amu unaopatikana kaunti ya Lamu katika pwani ya Kenya huvutia watalii wengi kwa utulivu wake na watu wanaopenda wageni.
Baadhi ya watalii hufika na baadaye wakaamua kuishi hapo.
Mmoja wao ni Hadija Ernest kutoka Marekani ambaye ameolewa na mwenyeji wa Amu.
Mwandishi wa BBC John Nene alikutana na Hadija pamoja na mumewe Bwanaadi Issa Ali ambaye ni mvuvi na amezungumza nao kuhusu maisha yao.