Kwa Picha: Maafa ya Kimbunga Matthew Haiti

Kimbunga Matthew ndicho hatari sana kutokea katika miaka ya hivi karibuni, kilisababisha mvua kubwa nchini Jamaica na visiwa vingine vya Caribbean.

Mwanamke ajifunika kwa kutumia karatasi ya plastiki kabla ya kuwasili kwa Kimbunga Mathew, Tambare Haiti.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Kimbunga Matthew - Kimbunga hatari zaidi kuwahi kukumba visiwa vya Caribean kwa kipindi cha miongo miwili - kimesababisha upepo mkali, mvua na dhoruba Haiti.
Raia wa Haiti wakiwa kanisani baada ya kuokolewa kutoka kwenye eneo lililo karibu na mto Grise kabla ya kuwasili kwa Kimbunga Mathew, Tabarre, Haiti,

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Serikali imejenga makazi 1,000 - kuwasitiri watu 340,000.
Wafanyikazi wa umma wawaomba raia kuondoka eneo lililo karibu na mto Grise Tabarre, Haiti

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Saa chache kabla ya kuwasili kwa kimbunga Matthew, raia wa Haiti walitakiwa kuondoka nyumbani mwao.
Msichana mdogo aangalia wakati maafisa walipofika kuondoa familia yake Tabarre, Haiti.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Raia wengine walikataa kuondoka, wakiogopa mali yao kuibwa
Mama ambeba mwanawe, wakati zoezi la kuhamisha raia likiendela kutokana na hatari ya mto ulio karibu kuvunja kingo zake, katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, tarehe 4 , Oktoba 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata familia zinazoishi kando ya mto zilikuwa zikikataa kuondoka
Mwanamke avalia kofia ya plastiki kabla ya kuwasili kwa Kimbunga Mathew mjini Les Cayes, Haiti, Oktoba 3, 2016.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kimbunga hicho kilitabiriwa kwamba kingesababisha upepo unaovuma kwa kasi ya 230km/h na kusababisha mvua ya kiwango cha inchi 40.
Hali ilivyo wakati kimbunga Mathew kikikaribia Port-au-Prince, Haiti

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Haiti inashuhudia na viwango vya juu vya umaskini na majanga. Hili ni jiji kuu, Port-au-Prince.
Mtoto akicheza nje ya nyumba yao kwenye mtaa wa mabanda mjini Port-au-Prince, Haiti

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Majengo hayajaafikia viwango vinavyohitajika vya ujenzi
Mwanamke asukuma toroli iliyojaa mali, kwenye mtaa uliofurika maji mjini Port-au-Prince, Haiti, tarehe 4 Oktoba 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raia katika maeneo yaliyofurika wakiokoa mali yao.
Afisa mlinzi asimama karibu na maduka yaliyofunikwa kwa kutumia mbao, kabla ya kuwasili kwa kimbunga Mathew mjini Kingston, Jamaica, Jumatatu Okt. 3, 2016

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Nchini Jamaica, wamiliki wa maduka walifunga maeneo yao ya kazi kabla ya kuwasili kwa kimbunga hicho.
People who were evacuated from their homes are seen in a room at a soccer stadium being used as a shelter while Hurricane Matthew approaches Kingston, Jamaica October 3, 2016.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu waliookolewa kutoka nyumbani mwao mjini Kingston walipewa hifadhi kwenye uwanja wa michezo.
Raia wa Jamaica wapiga picha ufuoni, wakitazama mawimbi yanayosababishwa na Kimbunga Mathew, viungani mwa Kingston.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Selfie na Kimbunga Mathew viungani mwa Kingston.
Raia wa Cuba wakiwa na mali yao wakiondoka kabla ya kuwasili kwa kimbunga Mathew.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Raia wa Cuba wajiandaa kabla ya kimbunga Mathew kuwasili.
Mwanamke akiwa kwenye hifadhi mjini Guantanamo, Cuba, kabla ya kuwasili kwa kimbunga Matthew, 3 Oktoba 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa kwenye hifadhi mjini Guantanamo, Cuba, kabla ya kuwasili kwa kimbunga Matthew.