Kwa Picha: Miaka ya Pitt na Jolie wakiwa pamoja

Tizama maisha ya Brad Pitt na Angelina Jolie walipokuwa pamoja wakati hisia mbali mbali zinaendelea kuibuka kufuatia tangazo kuwa Jolie ametaka talaka baada ya kuwa pamoja kwa miaka 12.

Brad Pitt na Angelina Jolie

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Uhusiano wa Jolie na Pit umevutia wengi katika vyombo vya habari kimataifa.
Angelina Jolie na Brad Pitt

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Walifurahia kuwepo katika maonyesho ya filamu zao pamoja ikiwemo filamu ya Ocean's 13 aliyoigiza Pitt 2007.
Angelina Jolie na Brad Pitt

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jolie akiwa mja mzito wa pacha wao Knox na Vivienne alipohuhuduria tamasha la filamu la Cannes 2008.
Angelina Jolie na Brad Pitt

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Wapiga picha kazini: wana ndoa hawa waliwavutia wengi kokote walikokwenda.
Angelina Jolie

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, 2010 Jolie alizuru Bosnia kama balozi mwema katika UNHCR pamoja na mumewe Pitt [ameipa picha mgongo].
Brad Pitt na Angelina Jolie

Chanzo cha picha, Getty_AFP

Maelezo ya picha, Pitt na Jolie wana watoto 6 pamoja wakiwemo 3 walio wa asili.
Angelina Jolie na Brad Pitt

Chanzo cha picha, AFP/Getty

Maelezo ya picha, Jolie alihudhuria mkutano wa kimataifa wa kupinga unyanyasaji wa kingono katika mizozo London Juni 2014, katika wadhifa wake wa mjumbe maalum wa UN.
Angelina Jolie na Brad Pitt

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wameigiza pamoja katika filamu By the Sea na wanaonekana hapa wakiwasili katika kuonyeshwa mara ya kwanza filamu hiyo Hollywood Novemba 2015.
Brad Pitt na Angelina Jolie

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Pitt na Jolie walijitambulisha rasmi kama wapenzi 2004, na wakaoana miaka 10 baadaye - mwaka picha hii ilipopigwa.
Brad Pitt na Angelina Jolie

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Taarifa za kutalikiana kwao zimejiri wakati kukiwa na ripoti kuwa Jolie anataka akabidhiwe watoto wao 6 awalee huku Pitt apewe haki ya kuwatembelea. wanaonekana katika picha hii Novemba 2015.