Kwa Picha: Kusherehekea utamaduni wa pwani Kenya

Nchini Kenya, mipango ya kukuza umoja baina ya makabila mbalimbali inaendelea kushika kasi huku taifa hilo likijiandaa kufanya uchaguzi mkuu mwaka ujao

Wakenya wakicheza ngoma asilia
Maelezo ya picha, Miguu yao ilitifua vumbi ngoma ilipogonga. Viuno vyao vilinenguka jinsi vyombo vya muziki vilivyopigwa ya ngoma zao asilia
Wanenguaji
Maelezo ya picha, Nyuso zao zilidondoka jasho kwa miondoko yenye mihemko. Kwa siku tatu mfululizo, Mombasa ilikuwa makao ya utamaduni cheshi kutoka kote nchini Kenya.
waziri na wanenguaji
Maelezo ya picha, Waziri wa utalii wa kaunti ya Mombasa, Binti Omar alikua mmoja wao na kando yake ni wakina dada walio miguu tupu wakikatika huku na kule
kundi la utamaduni
Maelezo ya picha, Watu wa mbali mbali walijitokeza kuonyesha utamaduni wa kila aina hususan ule unaopatikana maeneo ya pwani ya kenya
mama wa kipokomo
Maelezo ya picha, Karibu kidogo na eneo la ngoma kulikua na mama huyu mama kutoka jamii ya Wapokomo akiandaa mboga. Huku moshi ukitifuka kutoka motoni, mama anamwaga bakuli zima la nyanya ndani ya sufuria ya mchuzi
Wacheza ngoma
Maelezo ya picha, Wake kwa waume kutoka makabila mbali mbali ya Kenya walijumuika katika tamasha hilo la kitamaduni lililosifiwa sana na watu wa kabila zote
Bidhaa za kitamaduni zikionyeshwa
Maelezo ya picha, Licha ya ngoma na chakula bidhaa mbali mbali zinazotengenezwa kijadi pia zilionyeshwa kwenye tamasha hilo
Mapishi ya mboga
Maelezo ya picha, Ufundi wa mapishi ya mboga zinazoliwa na makabila mbali mbali nchini Kenya ni jambo lililowavutia walioshiriki tamasha hilo