Kwa Picha: Tetemeko la ardhi Italia

Tetemeko kubwa la ardhi limetokea katikati mwa Italia na kusababisha uharibifu mkubwa. Watu 38 wamefariki na wengine 150 hawajulikani walipo.

Maafisa wakiendelea na uokoaji

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter.
Vifusi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu wengi wamefariki maeneo ya Accumoli, karibu na kitovu cha tetemeko, na eneo jirani la Amatrice.
Maafisa wakiendelea na uokoaji

Chanzo cha picha, CORPO FORESTALE

Maelezo ya picha, Kijiji cha Pescara del Tronto kiliharibiwa kabisa na idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Maafisa wakiendelea na uokoaji pamoja na waathiriwa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Tetemeko la ardhi lilitokea eneo lililo katikati mwa Umbria, Lazio na Le Marche. Mitetemeko ilisikika maeneo ya mbali hadi Bologna upande wa kaskazini na Naples upande wa kusini.
Waathiriwa wakisaidiwa

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Juhudi za uokoaji bado zinaendelea. Watu wengi wanahofiwa kufukiwa kwenye vifusi.
Uharibifu uliotokea

Chanzo cha picha, Google / EPA

Maelezo ya picha, Picha hizi zinaonesha hali ilivyokuwa kabla na baada ya tetemeko la ardhi katika mji wa Amatrice.
Uharibifu uliotokea

Chanzo cha picha, Google / EPA

Maelezo ya picha, Picha hizi zinaonesha hali ilivyokuwa kabla na baada ya tetemeko la ardhi katika kijiji cha Pescara del Tronto.
Uharibifu uliotokea

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waziri mkuu Matteo Renzi amewashukuru watu waliojitolea kusaidia juhudi za uokoaji pamoja na maafisa wa uokoaji. Ameahidi kwamba walioathiriwa watasaidiwa.