Baby Shark ndio wimbo uliotizamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube
Bila shaka umeskia wimbo wa Baby Shark. Ni wimbo unaotumbuiza watoto kote duniani hivyo kujipatia umaarufu mkubwa sana tangu uliporekodiwa na kampuni ya kurekodi kutoka Korean ya Pinkfong. Sasa basi amini usiamini wimbo huu ndio uliotizamwa mara nyingi Zaidi kwenye mtandao wa Youtube ikiwa ni Zaidi ya mara bilioni 7.4.