EPL: Je, Edinson Cavani ndiye muokozi wa Manchester United?
Dirisha la uhamisho tiyari limefungwa katika ligi kubwa za Ulaya.Klabu ya Manchester United imemsajili mshambuliaji wa zamani wa Paris St-Germain Edinson Cavani kwa uhamisho huru. Mshambuliaji huyo ambaye aliondoka PSG Mwishoni mwa mwezi June na ambaye hakua na timu amesaini mkataba wa mwaka mmoja.