Raia Namibia waonywa kutumia kinyesi cha ndovu kama "tiba" ya Covid 19

Maelezo ya sauti, Raia Namibia waonywa kutumia kinyesi cha ndovu kama "tiba" ya Covid 19

Waziri wa Afya wa Namibia Kalumbi Shangula amewaonya watu dhidi ya kutumia vinyesi vya ndovu "kuponya" Covid-19. Waganga wengine wanasema kinyesi cha tembo kinaweza kuchemshwa na mvuke wake kutumika kama tiba ya homa, na maumivu ya kichwa lakini hili halijafanyiwa majaribio ya kisayansi. Nini maoni yako kuhusu hili? Sema nasi kwenye ukurasa wa Facebook, BBCSwahili.