Wagonjwa wa upasuaji Uingereza kuhudumiwa kupitia programu ya simu

Maelezo ya sauti, Madaktari Uingereza waibua njia mbadala ya Matibabu ya upasuaji

Janga la Corona limesababisha wagonjwa wengi wanaohitaji upasuaji kucheleweshewa huduma hiyo muhimu ili kuwapa kipaumbele wagonjwa wa virusi vya corona. Kwa sasa madaktari Uingereza wametafuta njia mpya mbadala ya kuwasaidia wagonjwa wa upasuaji kwa kutumia programu ya simu. Nini maoni yako kuhusu taarifa hii ? Sema nasi.