Dawa ya Dexamethasone kusaidia wagonjwa wa Corona.

Maelezo ya sauti, Dawa ya Dexamethasone kusaidia wagonjwa wa Corona walio mahututi

Hatimaye wataalam wa afya wamesema kwamba dawa aina ya Dexamethasone ambayo ni bei rahisi na kupatikana kwa urahisi pia,inaweza kusaidia maisha ya wagonjwa wa virusi vya corona walio mahututi.Wataalam wa Uingereza wanasema dawa hiyo ni hatua kubwa iliopigwa katika kukabiliana na virusi hivyo hatari.Mtafiti anaeongoza uchunguzi huo profesa Martin Landray anaeleza.