Mwanamziki wa mdundo wa 'Rock and Roll' Little Richard afariki dunia
Muimbaji aliyehamasisha kwa kaisi kikubwa mdundo aina ya rock 'n' roll mwimbaji Little Richard amefariki akiwa na umri wa miaka 87, familia ya mwanamuziki huyo imethibitisha. Wimbo wake maarufu Golly Miss Molly uliingia kwenye chati za nyimbo bora mwaka wa 1958. Nyimbo zingine zinazojulikana ni pamoja na Tutti Frutti na Long Tall Sally.