Wanaume wanne walioshtakiwa kwa ubakaji na mauaji wanyongwa nchini India
Wanaume wanne raia wa India wameuawa kwa kunyogwa nchini humo baada ya kushtakiwa kwa ubakaji na mauaji ya kinyamama kwenye basi huko Delhi mwaka wa 2012. Hatua hii imejiri baada ya rais wa India na mahakama kuu kutupilia mbali rufaa yao ya mwisho ya kusamehewa. Nini maoni yako kuhusu hukumu ya kifo? Sema nasi kwenye ukurasa wa Facebook, wa BBCSwahili.
