Mwanamziki wa Lingala Aurlus Mabele ameaga dunia
Mwanamziki wa nyimbo za Lingala Aurlus Mabele amefariki akiwa na umri wa mika 67. Kupitia mtandao wa twitter mwanawe Mabele kwa jina Liza Monet’ amedhibitisha habari za kifo cha babake. Mabele ni mwanamziki aliyevuma sana katika sekta ya muziki, mdundo wa lingala na vibao kadhaa ikiwemo cha Loketo.