Marufuku ya usafiri yameletea hasara kubwa sekta ya utalii

Maelezo ya sauti, Sekta ya utalii huenda ikafifia

Sekta ya utalii inaonya kwamba virusi vya corona vinaweza kuiletea sekta hiyo hasara ya milioni hamsini kote duniani. Baraza la usafiri na utalii duniani linataka hatua mbali mbali kuchukuliwa za kupunguza hasara mara tu virusi hivyo vitakapo dhibitiwa. Ndege, vikundi vya mahoteli na waendeshaji wa meli za baharini wamepata shida kubwa kutokana na vizuizi vikuu vya usafiri.