Faini itapunguza uenezaji wa habari za uongo kuhusu Covid19?

Maelezo ya sauti, Faini itapunguza uenezaji wa habari za uongo kuhusu Covid19?

Wakenya wako kwenye hatari ya kutozwa faini ya dola elfu 50 au kifungo cha miaka miwili iwapo watachapisha habari za uongo kuhusu mlipuko wa virusi vya korona. Mamlaka inasema imeongeza ufuatiliaji wa mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya dijitali kudhibiti kuenea kwa taarifa zisizo sahihi kuhusu ugonjwa huo. Nini maoni yako kuhusu hatua ya serikali ya Kenya? Sema nasi kwenye ukurasa wetu wa Facebook, BBCNewsSwahili