Je, ni kweli uhusiano kati ya Diamond Platnumz na Tansha umefika kikomo?
Mashabiki wa muziki wa bongo Flava hasa wale wa mwanamziki Diamond Platinumz wanaelezea maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhusiano wa Diamond na mwanamuziki kutoka Kenya Tanasha Donna. Hii ni baada ya Tanasha kufuta picha nyingi za Diamond kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram na pia kuacha kumfuata kwenye mtandao huo. Haya yanajiri siku chache tu baada ya wawili hao kutoa wimbo wao mpya wa Gere,uliopata umaarufu mkubwa mitandaoni.
