Mwanamuziki Joseph Shabalala afariki dunia

Maelezo ya sauti, Mwanamuziki Joseph Shabalala afariki dunia

Joseph Shabalala, ambaye alisaidia kutanguliza sauti ya muziki wa jadi wa Kizulu ulimwenguni, amefariki akiwa na umri wa miaka 78. Mwanamuziki huyo alijulikana sana kama mwanzilishi na mkurugenzi wa kikundi cha wanamuziki cha Ladysmith Black Mambazo,ambacho kilishinda tuzo tano za Grammy na kuhusishwa sana kwenye albumu ya Paul Simon ya Graceland.