Pele 'ahisi aibu kutokana na hali yake ya kiafya

Maelezo ya sauti, Pele 'aibika' kutokana na hali yake ya kiafya

Mchezaji maarufu wa soka nchini Brazil na ulimwengu kwa jumla Pele hayuko radhi kuondoka nyumbani kwake kwa sababu hawezi kutembea bila usaidizi.

Bingwa huyo mara tatu wa kombe la dunia, aliyejipatia sifa za kuwa mchezaji bora zaidi wa kandanda alipelekwa hospitalini akiugua maambukizi ya mkojo mwaka uliopita.