Nywele ndefu zampatia mtoto mvulana umaarufu mitandaoni

Maelezo ya sauti, Nywele ndefu zampatia mtoto mvulana umaarufu mitandaoni

Mtoto wa miaka saba Farouk James kutoka London amekuwa maarufu katika mtandao wa Instagram kutokana na nywele zake ndefu. Mtoto huyo ambaye ni mwanamitindo amepata umaarufu sana huku mamake akikashifiwa kwa kumruhusu mtoto wake kufuga nywele hizo. Yapi maoni yako kuhusu nywele ndefu kwa watoto wavulana? Tuwasiliane kwenye Facebook BBCSwahili