Akaunti za waigizaji wa ngono zaondolewa Instagram
Mamia ya akaunti za waigizaji wa filamu za ngono zimetolewa katika mtandao wa Instagram mwaka huu, huku wengi wakisema watu hao wako katika hadhi tofauti kuliko nyota wa kawaida. Mtandao huo umedai akaunti hizo huchapisha maswala yaliyo kinyume cha sheria za mtandao huo.