Wanafunzi wasio waislamu wahimizwa kuvalia hijab nchini Uingereza
Wasichana wa shule mmoja huko Uingereza wamehimizwa wavalie hijab kwa siku moja ili kuwahamasisha watu dhidi ya unyanyasaji. Hii ni baada ya wasichana walio na hijab kunyanyaswa huko Lincolshire. Mwanaharakati Ghada Mohamed anataka kutumia mbinu hiyo ili kuihamasisha jamii.
Je, ubaguzi wa kidini hushuhudiwa nchini mwako?
Tujadiliane kwenye Facebook BBCSwahili.com