Mwanaharakati wa Tanzania, Maria Sarungi alitekwa nyara katika mazingira gani?
Mwanaharakati wa Tanzania, Maria Sarungi alitekwa nyara katika mazingira gani?
Taarifa za kutekwa kwa mwanaharakati Maria Sarungi wa Tanzania zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii Jumapili jioni. Hii ni baada ya taarifa iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International nchini Kenya kabla ya yeye mwenyewe kuchapisha ujumbe kwenye akaunti yake ya X. Maria alihakikisha kwamba yuko salama na atazungumza zaidi juu ya kutekwa kwake siku ya Jumatatu.
Lakini kwa sasa hali yake ikoje? Na alitekwa kwenye mazingira gani?
BBC imezungumza na Roland Ebole wa Amnesty International nchini Kenya.
