Paul Makenzie: Mama yangu alikufa, dada yangu sijui kama yupo hai’’
Miili ya watu zaidi ya 80 wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa madhehebu ya Kikristo walioamini kuwa wangeenda mbinguni ikiwa wamefunga hadi kufa ilifukuliwa katika msitu huko nchini Kenya
Ndugu wa waathiriwa wa mkasa wa kanisa tata nchini Kenya amesema alimpoteza mama yake na dada yake hajui alipo.
Akizunguza na BBC anasema alijaribu kuwaonya juu ya kujiunga na kanisa hilo.
Idadi ya waliofariki, ambayo imekuwa ikiongezeka kwa kasi katika muda wa siku mbili zilizopita huku uchimbaji ukiendelea, inaweza kuongezeka zaidi kwani Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema watu 112 wameripotiwa kupotea kwenye dawati la ufuatiliaji wanaloendesha.
Ibada hiyo iliitwa Good News International Church na kiongozi wake, Paul Mackenzie, alikamatwa kufuatia taarifa iliyodokeza kuwapo kwa makaburi yenye kina kirefu yenye miili ya wafuasi wake 31.
Miili ya watoto ilikuwa miongoni mwa waliofariki. Polisi walisema uchimbaji wa makaburi mengine ili kutafuta miili zaidi unaendelea. Kiongozi wa kanisa hilo, Paul Makenzie Nthenge yuko rumande, akisubiri kufikishwa mahakamani.

Chanzo cha picha, EPA
