Uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam: Serikali ya Tanzania yazungumza
Uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam: Serikali ya Tanzania yazungumza

Chanzo cha picha, Reuters
Serikali ya Tanzania imejikuta ndani ya mjadala mzito wenye misingi ya uwekezaji katika bandari za nchi hiyo, ambazo ni moja ya rasilimali muhimu za kiuchumi, huku Mamlaka ya usimamizi wa Bandari TPA ikilazimika kutoa taarifa ya ufafanuzi kwa umma usiku wa kuamkia hii leo.
Awali nimezungumza na msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa kutaka kufahamu Je ni kweli kwamba kampuni ya DP World inakuja kuchukua shughuli zote za bandari nchini Tanzania?