Bendi ya Wasiiona iliyoteka Mitaa ya Dar es Salaam kwa burudani

Chanzo cha picha, Getty Images
Muda wa kusoma: Dakika 1
Ulemavu umewanyima wengi fursa ya kuonesha ukubwa na ubora wa karama walizo jaaliwa, lakini kwa Daniel Maige na kundi lake ulemavu sio ukingo, kwani licha ya kutoona wanatumia vipawa vyao vya muziki kutunga nyimbo na kupiga ala mbalimbali za muziki kwenye Barabara za Jiji la Dar es salaam.
Kwa Mara ya kwanza Daniel na wenzake walingia barabarani mwaka 2015 na tangu wakati huo hadi hii leo wanaendelea kuudhiirishia ulimwengu kuwa wamejaliwa karama za kipekee licha kukabiliana na changamoto mbalimbali kama vile usafiri, uchakavu wa vifaaa na hata kadhia ya kufurushwa na askari wa jiji baadhi ya maeneo.
Mwandishi wa BBC Eagan Salla aliwatembelea na kuandaa tarifa ifuatayo.









