Miaka 65 ya BBC Swahili: Vicky Ntetema 'wanahabari wanapoona kuna ugumu wasikate tamaa'

Maelezo ya sauti, Wanahabari hata wanaopoona kuna ugumu wa kufanya jambo fulani wasikate tamaa

Vicky Ntetema ni mmoja wa wanahabari wa kike ambao ni tajika hasa wakati alipokuwa mtangazaji wa BBC Swahili.

Hali kadhalika Vicky anafahamika kwa kuwa mwanahabari wa kike ambaye alihusika na upekuzi wa jinsi watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi au Albinism walivyokuwa wanauawa nchini Tanzania kwa kile kiliaminika na baadhi ya watu wa vijijini kuwa kutafuta nguvu za kishirikina.

Vicky alishinda tuzo la kimataifa la International Woman of Courage kwa upekuzi huo kuhusu ulemavu wa ngozi.

Wiki hii ambayo BBC Swahili inaadhimisha miaka 65 tangu kuanza matangazo yake ya kwanza, naye anaadhimisha miaka 64 tangu kuzaliwa kwake.

Anne Ngugi alipata fursa ya kuzungumza naye kwa njia ya simu akiwa London ambapo ndio makao yake ya kwanza na kuanza kwa kumuuliza anakumbuka vipi BBC wakati huo na sasa, hebu tumsikilize...