Unaufahamu mlio wa sauti ya 'hewa chafu' ya Sokwe?
Kwa miongo kadhaa sasa Sokwe wa milimani wamekuwa katika hatari ya kutoweka. Aina hiyo ya sokwe wameorodheshwa kama wanyama walio "hatarini" - kutoweka. Mhariri wa hali ya hewa wa BBC, Justin Rowlatt, alienda katika msitu wa Bwindi Impenetrable, Uganda ili kujua kuhusu uhifadhi sokwe wa milimani na kupata zaidi ya alichokifuata alipokaribiana na wanyama hao.
