Maisha katika nyuzi joto 50: Fahamu jinsi unavyoweza kupoza nyumba yako kwa urahisi
Joto kali imekuwa kawaida nchini India kutokana na ongezeko la joto duniani. Hakuna pa kujificha haswa ikiwa unaishi kwenye makazi duni.
Shakeela Bano anajitahidi kumfanya mjukuu wake Mohammed alale katika nyumba yao ya chumba kimoja.
Lakini kama mfululizo wa makala za Maisha katika nyuzi joto 50 kuhusu mabadiliko ya hali ya tabia nchi inagundua, kuna suluhisho moja ambalo haliigharimu dunia.