Robert Burale: Kocha anayewafunza wanawake jinsi ya kujipatia wapenzi wapya

Maelezo ya video, Robert Burale: Kocha anayewafunza wanawake jinsi ya kujipatia wapenzi

Mafunzo ya mapenzi na mitindo ya maisha ni sekta inayotengeneza mabilioni ya madola na moja inayokuwa kwa kasi kubwa zaidi. Watu wengi wasio na wapenzi wanatafuta wapenzi. Hivyobasi hali hiyo imesababisha ongezoko la walimu wanaosambaza kanda chungu nzima za video mbali na mafunzo ya kibinafsi yanayogharimu fedha nyingi. BBC imekutana na mmoja ya walimu wa mapenzi na mitindo ya maisha , Robert Burale , katika hafla ambayo anawaahidi wanawake kwamba watapata mabwana ifikiapo siku kuu ya Krisimasi.