'Matamshi ya IGP yanaondosha mazingira ya maridhiano'-ACT
Baadhi ya vyama vya upinzani nchini Tanzania vimesema havitahudhuria mkutano wa jeshi la polisi na vyama vya siasa ulioitishwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa.
Mkutano uliitwa kujadili njia za jinsi ya kuboresha mazingira ya kisiasa nchini Tanzania, lakini upinzani unasema mkutano huo hautakuwa na athari yoyote ikiwa waziri anayesimamia usalama wa ndani hawezi kuhudhuria. Mahojiano na Katibu mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu.