Siku 100 za Rais Samia Suluhu: Awamu mpya na deni la kuendeleza miradi
Moja ya maswali makubwa ambayo wengi walijiuliza baada ya kifo cha Rais John Magufuli nchini Tanzania lilikuwa ni: ipi hatma ya miradi ya maendeleo aliyoianzisha?
Mrithi wake, Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendeleza miradi yote ya kielelezo ya mtangulizi wake, na ujenzi wa reli ya SGR ni kielelezo muhimu.