Yasmine Agbantou, mwanamke aliyeamua kubuni mitindo nguo za wanawake wanene
Mbunifu wa mitindo Yasmine Agbantou ni mwanamke anayetengeneza mitindo ya wanawake wanene na akiwa mnene mwenyewe alichoshwa na kuona mavazi ya fasheni ya kifahari yanatengenezwa kwa kuwafikiria wanawake wenye maumbo madogo.
Baada ya kujifunza mbinu za fasheni katika majumba makubwa ya fasheni, mbunifu huyo kutoka Afrika Magharibi alibuni nembo Minimine AG. Anasema ‘’Uasi’ wake wa hivi karibuni wa mavazi unatoa’’nguo za kifahari na za kisasa’’ zilizobuniwa kwa ajili ya wanawake wanene’’ kwa lengo la kuwafanya’’ wajihisi vizuri na wenye muonekano mzuri’’