Matokeo ya Uchaguzi Uganda 2021:Bobi Wine ataka watu wasubiri majibu kutoka kwa mawakala
Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Uganda, huku rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 akiwa anaongoza katika matokeo ya awali. Bobi Wine ambaye alikuwa na wafuasi wengi vijana anasema atawaarifu watu kitakachofuata baada ya wakala wake kuja na majibu.
