Billboard: Albamu ya Evermore ya Taylor Swift yasalia nambari moja.
Albamu ya mwanamziki Taylor Swift aliyoizindua ghafla wakti wa janga la Corona ya Evermore, imevunja rekodi ya kusalia kwa nambari moja kwenye chati ya muziki ya Billboard. “Evermore,” ambayo ilizinduliwa wiki nne zilizopita imekuwa na mauzo ya elfu 56,000 nchini Marekani kuilingana na kampuni ya mauzo ya muziki ya Nielsen Music/MRC.
