'Niliweka tattoo ili niwe na alama sawa na mwanangu'

Maelezo ya video, 'Niliweka tattoo ili niwe na alama sawa na ya mwanangu'

Derek Prue, kutoka Alberta nchini Canada, aliamua kwenda kuchora tatoo ambayo inafanana na alama ambayo mtoto wake wa kiume mwenye miaka nane anayo.

Baba huyo alifikia maamuzi hayo baada ya kumuona mwanae kuwa anahofia kuwa na alama ya kuzaliwa katika mwili wake na yeye alitaka kumuonesha kuwa ni jambo la kawaida kabisa.