Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Apple awa bilionea.
Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya teknolojia ya Apple Tim Cook amejiunga na kundi la mabilionea bada ya bei ya hisa ya kampuni hiyo kuongezeka maradufu.Cook anamiliki hisa 847,969 moja kwa moja na kupata faida ya dola milioni $ 125m mwaka jana kama sehemu ya malipo yake.
