Mji wa Shenzhen nchini China waweka marufuku ya ulaji wa paka na mbwa

Maelezo ya sauti, Mji wa Shenzen nchini China waweka marufuku ya ulaji wa paka na mbwa

Mji wa Shenzhen umekuwa mji wa kwanza nchini China kupiga marufuku ya uuzaji na ulaji wa nyama ya mbwa na paka. Hatua hii inakuja baada ya ugonjwa wa virusi vya corona kuhusushwa na wanyama pori hivyo kulazimu mamalka kupiga maarufu biashara ya wanyamapori. Shenzhen hata hivyo imeongeza marufuku hiyo kwa mbwa na paka...sheria hii mpya itaanza kutekelezwea Mei Mosi. Mbwa milioni thelathini huuwawa kila mwaka barani Asia kwa minajili ya nyama.