Erick Kabendera alikuwa nguzo ya matibabu ya mama yake
Mama wa mwandishi wa habari aliye mahabusu nchini Tanzania Erick Kabendera amefariki dunia siku chache baada ya kutuma ujumbe kwa rais Magufuli kupitia vyombo vya habari
Bi. Verdiana Mjwahuzi (81) alitoa hisia zake ni namna gani maisha yake yalivyo magumu bila ya mwanae Erick Kabendera.
Mama huyo amefikwa na umauti katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumanne.
